Ijumaa, 26 Mei 2017

Wasanii vinara kwa ushirikina watajwa

Meneja wa wasanii wa bongo fleva maarufu kwa jina la Meneja Maneno, amefunguka na kusema wapo wasanii wengi Bongo wanaamini ushirikina na kukiri kuwa wapo wasanii wengine ambao yeye mwenyewe aliwapeleka kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kuroga.

Meneja Maneno aliyewahi kuwa meneja wa Diamond Platnumz, Rich Mavoko, Sam wa Ukweli na Nay wa Mitego, amefunguka hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kuwataja wasanii ambao aliwahi kuwapeleka kwa waganga na ambao wanaamini sana ushirikina kuwa ni pamja na Rich Mavoko, Sam wa Ukweli huku akisema katika wote Diamond Platnumz ndiyo zaidi yao. 
"Ndele ni sehemu ambayo baadhi ya wasanii waliiamini sana lakini Mungu akisema 'Yes' ni 'Yes' tu kwa hiyo nakumbuka wasanii ambao nilikwenda nao kwa waganga kuroga ni pamoja na Rich Mavoko tena tulienda mbali kabisa huko Kigamboni ndani ndani huko tumeenda ndugu yangu, nilisharusha nazi katikati yaani usiku ule unajifanya chizi kama umevurugwa" alisema Meneja Maneno
Meneja Maneno
Meneja Maneno aliendelea kutoa orodha ya wasanii hao ambao kwao shiriki ni kitu ambacho wanakiamini na kukiri kwenda nao huko na kufanya mambo hayo 
"Hata Sam wa Ukweli siwezi kukataa, ni watu ambao imani yao iliwapeleka huko lakini mimi nakumbuka kazi yangu niliyokuwa nafanya sikutaka kwenda kwa waganga.... ila sasa huyu Mondi sasa nimepata taabu naye, mara leo twende kwa mjomba, tunapeleka unga, leo tunapeleka mchele na mganga alivyo mshenzi hajawahi kuagiza samaki, yeye ni jogoo, mbuzi" alisisitiza Meneja Maneno

Mzee Yusuph ataka nyimbo zake zifutwe

Aliyekuwa mfalme wa muziki wa miondoko ya pwani 'taarab', Mzee Yusuph amewataka watu wote waliokuwa na nyimbo zake kwenye simu wafanye hima kuzifuta kwa madai wakiendelea kuzisikiliza watampatisha dhambi katika hilo.



Mzee Yusuph
Mzee Yusuph amefunguka hayo ikiwa ni masaa machache yamebakia kwa waumini wa dini ya kiislamu kuanza ibada yao ya kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.
"Mimi nikikubali watu wacheze nyimbo zangu ina maana nimeruhusu dhambi tena ni bora nirudi kuimba muziki tena, hivyo watu wote waliokuwa na nyimbo zangu kwenye simu zao wafute na kuacha kusikiliza ili kuepuka dhambi....Nimetenda sana makosa tena hadharani na kila mtu anajua lakini kwa sasa ninawaomba tu mniombee dua ili niendelee kuwa salama japo hali yangu kiuchumi haiko sawa imebadilika nazidi kupambana ili kipatikane kitu" alisema Mzee Yusuph
Aidha, Mzee Yusuph amesema kwa sasa hajihusishi na masuala ya muziki wa kidunia tena bali ataendelea kuitangaza dini yake pamoja na kuimba nyimbo za kaswida.
Pamoja na hayo, Mzee Yusuph amewasihi waislamu kumrudia Mungu wao kwa kufanya mambo mema katika kipindi hiki cha mfungo pamoja na kuwataka akina baba kuacha manyanyaso kwa wake zao majumbani.

Habari IGPost Maneno ya Wema Sepetu baada ya kifo cha Ivan Semwanga, mzazi mwenzake na Zari….

Miss TZ 2006, TZ Sweet Heart, Wema Sepetu ni miongoni mwa mastaa wa bongo walioguswa na msiba wa Ivan Semwanga, Baba watoto watatu wa Zari na Kupitia IG yake alitoa haya maneno kwaajili ya familia ya Ivan, watoto na mama watoto ambaye ni Zari The Boss Lady.
Ujumbe wa Wema ulikuwa Hivi….”Broken hearted…… Rest In Peace Ivan… … SHOCKING NEWS kwakweli… My Condolences to The whole Family… Mungu awatie nguvu wale watoto jamani… They are too young… And Mungu amtie nguvu Mama watoto wako… It will be a very hard period of time for all of you But it shall pass…“
Picha ya Dj Amani the  mixx masters

BURUDANIJacqueline Wolper kajibu kama amewahi kujutia kuwa na mahusiano na Harmonize….

Kwenye #KikaangoniEATV Msanii wa filamu maarufu Tanzania Jacqueline Wolper amefunguka juu ya mahusiano yake maarufu sana na msanii wa WCB Wasafi Harmonize.
Wolper aliulizwa kama anajutia kuwa na Harmonize baada ya kuachana naye…
Wolper anasema Sio Kila kilichotokea kati yake ni Harmonize ni kibaya….

BURUDANIRihanna na Lupita Nyong’o kwenye filamu mmoja, NI VIBAKA….

Mshindi wa tuzo ya Oscar Lupita Nyong’o na Rihanna wataigiza kwenye filamu mpya ya ujambazi itakayoongozwa na Ava DuVernay (Selmana kuandikwa na Issa Rae (“Insecure”). Filamu hii itakuwa chini ya kampuni ya Netflix.
Filamu hii imepata ushawishi mkubwa kutoka kwenye picha ya mwaka 2014 ya Rihanna na Lupita kwenye onyesho la mavazi la Miu Miu.
Blogger maarufu kwenye mtandao wa #Tumblr ‘Elizabitch Taylor‘ alipost picha hii nakuandika ‘They look like they’re in a heist movie with Rihanna as the tough-as-nails leader/master thief and Lupita as the genius computer hacker.
Picha hii ilisamba sana mitandaoni na kupata NOTES 470,000.

BURUDANIBillnass; Kufanya muziki na chuo nimepoteza pesa nyingi sana…..

Msanii Billnass ambaye pia ni mwanachuo CBE Dar es salaam ameongelea pesa alizopishana nazo wakati yupo masomoni nakudai alibidi aweke pembeni show ili kupiga kitabu.
Billnass anasema “Kufanya muziki na chuo nimepoteza pesa nyingi sana, watu wengine hawawezi kujua, nimeshakataa ‘show’ nyingi sana, nimeshaacha kwenda kwenye matamasha kibao…Vitu vingi sana vya kimuziki vilinipita na ndiyo ilikuwa ‘time’ yangu, kipindi cha ‘Chafu pozi’ inawika nilikuwa napata dili nyingi sana yaani hela ambayo najua kabisa hata nikimaliza chuo nisiweze kuitengeneza lakini masomo yalinibana zaidi“. 
Billnass akiwa shule ameweza kutoa hits kubwa kwenye radio na tv kama Raha na Chafu Pozi.

BURUDANIPicha,Wiz Khalifa akutana na Sylvester Stallone….

 Rapa Wiz Khalifa ametimiza ndoto yake ya kukutana na staa wa filamu aliyemtazama kwenye tv toka akiwa mtoto kwenye filamu kubwa kama Rocky na RAMBO.
Staa huyu wa filamu ni Sylvester Stallone na Wiz Khalifa hakupoteza muda na kupiga naye picha akionyesha ishara ya kumpiga ngumi kama wako kwenye filamu maarufu za Stallone #Rocky.

HABARI#IGPost, Maneno ya Diamond Platnumz baada ya kifo cha Ivan, mzazi mwenzake na Zari The Boss Lady…

Asubuhi ya May 25,2017 Afrika Mashariki iliamka na msiba mkubwa wa Ivan Semwanga baba watoto watatu wa Zari The Boss lady na mfanya biashara maarufu sana Uganda. Kifo chake kimegusa mastaa na mashabiki wengi wa bongo fleva.
Diamond Platnumz ambaye kwa sasa ndio mpenzi wa Zari na wana watoto wawili ameandika maneno haya baada ya kifo cha Ivan..”Mbele yako, Nyuma yetu…..”
Picha ya Dj Amani the  mixx masters
Picha ya Dj Amani the  mixx masters

Wengi wanapenda kumuita King Kiba (Yaani mfalm....................

Wengi wanapenda kumuita King Kiba (Yaani mfalme Kiba), je unadhani Alikiba anastahili jina hilo? NDIYO / HAPANAPicha ya Dj Amani the  mixx masters