Jumamosi, 27 Januari 2018

BURUDANI Fat Joe amchana Rais Donald Trump kuhusu kugawanyisha Raia. .

Rapa na staa wa HipHop kutoka mitaa ya Bronx, New York  Fat Joe amesema yeye sio shabiki wa Rais Donald Trump.
Fat Joe ambaye wazazi wake wanatoka Puerto Rico na Cuba anasema >“Sisi ndio sauti za raia wa Marekani, lazima tuongee kwa niaba yao, hii ndio HipHop, Trump aliwakimbia watu wangu Puerto Rico, hivi karibuni amewatukana na kuwakosea heshima watu wa Haiti, amegawanyisha nchi”.
Fat Joe yupo studio akirekodi album yake mpya ya Family Ties, producer ni Dre, wa Cool & Dre, inasemekana Jay-Z atasikika kwenye album hii pia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni