Ijumaa, 24 Februari 2017

Leicester City yamtimua kocha wake Claudio Ranieri


Uongozi wa klabu ya Leicester City umemtimua kocha wake Claudio Ranieri ’65’ ikiwa ni miezi 9 tangu aiongoze klabu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza.
Leicester imekuwa na msimu mbovu ikiwa imeshinda michezo 5 pekee, haijafunga bao lolote kwenye ligi tangu mwaka 2017 uanze na Pia wapo point moja na nafasi moja juu ya mstari wa kushuka daraja.
Kufukuzwa kwake kazi kumekuja saa 24 baada ya Leicester City kufungwa 2-1 na Sevilla kwenye Champions League.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni